Sunday, October 12, 2008


Get real meaning of Bongo fleva:
toka kwa Ibony Moalim: Neno Bongo ni neno linalotokana na maana kuu 2 ya kwanza ni ile tafsiri ya kuwa watanzania wengi huishi kwa kutumia akili (Bongo) yaani kwa watu waliokuwepo miaka ya 90 hili neno lilitumika sana kwa mfano mtoto huyu ni Bongo lala ni yule ambae hana akili, na Maana ya pili kutokana na hali ngumu ya watanzania tuliyokuanayo hasa baaba ya vita vya Kagera majirani zetu walitukejeli kuwa sisi ni wagumu kama vingoma vinavyotumika kwenye bendi za Orchestra maarufu kwa jina la Bongos, ugumu wa vigoma hivyo ndiyo tulifanishwa navyo. Twende kwenye neno Fleva ni neno la kingereza lenye maana ya vionjo.

Bongo fleva ni mtindo wa muziki ambao ulikuja na utandawazi miaka ya 90 wakati studio za kuandalia muziki zilipoingia, kwa sisi wa Dar es salaam ilikuwa ni Don Bosco Kwa Marlon/Amri hingi/Joshua Kyara /Richard mloka/John Ngosha hawa walikuwa maprodyuza, ukikosa hapo ni Magomeni kwa Mhuto na Prodyuza alikuwa ni Jerry/Joseph na George mhuto au unaweza kwenda Oysterbay kwa Master Jay kwenye kontena na prodyuza Alikuwa Master Jay/P funk/John Kagaruki au kwa Enriko Temeke Sound Crafters na maproduza walikuwa ni Enriques na Roy. au Mawingu Studio kwa prodyuza bonny lov/Kusaga Kipindi hiki studio zote walikuwa na mashine za kurekodi 4 track na wenye work station walikuwa wanaweza 'ku RE bauns' na kupa track 8, upeo wa maproduza ulikuwa mdogo sana na na hata vifaa vilikuwaduni Kwa wale wasanaii wa michezo ya kuigiza na Orchestra/Kwaya walikwenda RTD nao walikuwa na studio kwa Dar es salaam ndiyo ilikuwa studio kubwa pekee. (kumbuka wengine walitumia SPOOL yaani mikanda mikubwa kama ya kurekodia kwenye Sinema.

Ilipofika 96 kuliakuwa na utitiri wa "Home studios" nahapo ndipo ilipotokea maana ya Bongo fleva:
Ubunifu wa midundo ya muziki unatokana na vionjo ambayo hupatikana kwa kila aina ya mtindo wa muziki kwa mfano kuna vionjo vya Zouk, Orchestra Rhumba, Pop, R&B, Soul na vingine vingi,

KATIKA KUBUNI MUZIKI:
Kwa kawaida maproduyuza wanatakiwa kutumia staili moja ya muziki au kuchanganya staili 2 ili kutengeneza 'Fussion' yaani mchanganyiko wa aina mbili za mitindo ambao utaleta staili moja.

Kwa ajili ya utandawazi hapa kwetu ikawa kinyume na utaratibu wa kutengeneza 'Fussion' kutoka kwenye mitindo 2 ilikuwa ni Fussion ya mitindo zaidi ya 5 na maprudyuza wengi walikuwa waki Fluk na kupata muziki ambao hawakuutarajia ila unasikika vizuri wengine walitumia Sampler na wengine plugins ili kufanikisha zoezi hilo.

Maprodyuza studio hawakufahamu hiki ni kionjo cha Mtindo gani wa muziki kwahiyo walitupia tupia vionjo visinyopungua aina tano na kupata Fussion iliyozaa BONGO FLEVA , Upande wa wasanii ndio walichangia sana kuwapoteza maprodyuza wakiwa studio kwa kuwa kila kionjo walichowasikilizisha walidata nacho na kutaka kiwepo kwenye nyimbo kwa hiyo nyimbo moja itakuwa na vionjo mbalimbali Unaweza kukuta Drams(Rythm) inaenda Zouk lakini Bassline ya hiphip, Vinanda vya R&B muimbaji mwenyewe anaimba Rap hii 'Fussion' ndio iliyozaa BONGO FLEVA. Endelea kupitia tovuti hii utapata mengi kuhusu Bongo Fleva.

No comments: